Msimu huu hatuna nafasi ya kufanya makosa - Ahmed Ally
Eric Buyanza
October 26, 2026
Share :
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema msimu huu kikosi chao hakina nafasi ya kutofanya vizuri.
Ahmed amesema hivyo baada ya Simba kuwa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuongoza kwa pointi 5, huku wakiwa wamefuzu Hatua ya Makundi ya CAF.
“Msimu huu hatuna nafasi ya kufanya makosa. Baada ya kufanya ukatili kimataita sasa tunarejea rasmi kwenye ligi kuu ya NBC na aliye mbele yetu ni Fountain Gate, October 29 katika Uwanja wa Kwaraa Babati.
“Niwaombe sana Wanasimba sasa tuelekeze nguvu kwenye mechi za ligi tena nguvu ya sawa sawa pengo la point 5 kwenye msimamo wa ligi lituongezee nguvu, hasira na umakini wa kupambana zaidi. Macho kwenye NBC” ameandika Ahmed Ally.






