Msimu mbaya kwa Mayele
Sisti Herman
February 15, 2026
Share :

Nyota wa Klabu ya Pyramid na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fiston Mayele ameendelea kuandamwa na ukame wa kushindwa kutia mpira nyavuni kwa mechi zaidi ya 19 bila goli wala Assist.
Mara ya mwisho kwa Mayele kufunga goli ilikuwa ni October 25, 2025 ambapo alifunga goli 1 kwenye ushindi wa goli 2-0 walioupata dhidi ya Pharco FC kwenye ligi kuu Misri. Ikumbukwe kuwa Mayele ndo mchezaji aliyekuwa anatetea pia kiatu chake cha ufungaji kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika ila mpaka sasa hana goli lolote wala Assist kwenye michezo 6 ya makundi waliocheza Pyramid mpaka sasa.
Kinaweza kuwa kipindi kigumu kwa mchezaji huyu wa zamani aliyewaka sana mitaa ya Twiga na Jangwani kabla ya kutimkia kwa matajiri hao wa Misri.





