Msindo ajifunga Azam hadi 2027
Sisti Herman
April 3, 2024
Share :
Beki wa kushoto Azam Fc Paschal Msindo ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili zaidi baada ya leo kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili.
Msindo ambaye msimu huu amekua mwiba mkali kwenye mbinu za Dabo hadi sasa ana goli 1 na asisti 4 kwenye mechi 13 za ligi kuu.