pmbet

Msinilinganishe na Ronaldinho, huyo alikuwa gwiji - Okocha

Eric Buyanza

January 12, 2026
Share :

Nahodha wa zamani wa Super Eagles, Austin ‘Jay-Jay’ Okocha, amesema ni vigumu kumlinganisha yeye na nguli wa soka Ronaldinho, huku akikiri kwamba kati ya wachezaji aliowahi kucheza nao huyo ndiye mwenye kipaji zaidi.

Okocha alikuwa akichangia maoni yaliyotolewa na meneja wa Arsenal, Mikel Arteta, ambaye aliwahi kucheza na wachezaji hao wote wawili katika klabu ya Paris Saint-Germain, ambapo anasema yeye mwenyewe ilimpa ugumu kuamua nani mwenye kipaji zaidi kati ya wawili hao.

 

Okocha alisema: "Siwezi kusema kwamba kuna mtu yeyote ni bora kuliko mimi. Lakini Ronaldinho alikuwa gwiji linapokuja suala la soka" "Alileta kitu tofauti, na tulielewana kwa sababu msingi wetu ulikuwa sawa. Tulijifunza jinsi ya kucheza mitaani; tulikuwa tukicheza kwa sababu tuliupenda mchezo"
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet