Msitumie magari ya serikali kuendea Baa - Dkt Mpango
Eric Buyanza
July 9, 2024
Share :
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango amewaagiza wakuu wa wilaya za mkoa Kigoma kufuata maadili ya uongozi katika kutumia magari waliyokabidhiwa kwa kuleta tija katika kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyia kazi badala ya kutumia magari hayo kwenda baa.
DK Mpango amesema hayo Ikulu ndogo mjini Kigoma wakati akikabidhi magari kwa wakuu wa wilaya akiwa kwenye ziara ya kiserikali ya siku saba mkoani humo na kusema kuwa ni lazima magari hayo yatoe matokeo yanayopimika katika utendaji wa matumizi ya magari hayo.
Amesema amegundua bado wakuu wengi wa wilaya hawajui shida, kero na changamoto zilizopo kwa wananchi hivyo ni lazima magari hayo yatumike kufika kwa wananchi kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi.