Msuva atambulishwa rasmi Saudia
Sisti Herman
January 24, 2024
Share :
Klabu ya Al Najmah FC ya nchini Saudi Arabia imemtambulisha rasmi mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva ambaye yupo na Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2023 yanayoendelea Ivory Coast kuwa mchezaji wao mpya.
Msuva anajiunga na Al Najmah kama mchezaji huru mara baada ya mwishoni mwa mwaka jana kusitisha mkataba wa kuitumikia JS Kabylie ya Algeria.
Kila la kheri kwake.