Msuva awaweka njiapanda Yanga
Sisti Herman
January 10, 2024
Share :
Inasemekana jaribio lingine la Yanga kuwania saini ya winga hatari wa Taifa Stars Simon Msuva limewaacha njiapanda wananchi baada ya Msuva kuwataka mabosi wa timu hiyo kuendelea kusubiri kwani anaamini kuwa anaweza kupata timu kwenye ligi kubwa baada ya AFCON
Msuva ambaye kwasasa ni mchezaji huru ameamua kuwapa jibu hilo Yanga kwani anaamini wachezaji wengi huonekana kupitia AFCON hivyo anaamini michuano hiyo pia bado inaweza kumfungulia njia kwenye ligi zingine baada ya Algeria na Morocco.