Msuva hawezi kukataa kurudi nyumbani - Arafat
Sisti Herman
December 28, 2023
Share :
Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga Arafat Haji amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mipango ya timu hiyo kwenye dirisha hili la usajili huku akigusia suala la klabu hiyo kuhusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Taifa Stars Simon Msuva.
“tumejipanga kutambulisha watu wetu Zanzibar kwenye Mapinduzi Cup, Msuva ni mchezaji mzuri, Tanzania ni nyumbani kwa Msuva kama kuna vilabu vitamtaka sidhani kama atakataa kujiunga nyumbani, sisi tuna mipango yetu nadhani ndani ya siku 7 zijazo tutatangaza” alisema Arafat kwenye mahojiano ya ana kwa ana na PM Sports.
Yanga hadi sasa imemtambulisha mchezaji mmoja tu, Shekhan Ibrahim kutokea JKU ya Zanzibar.
Fuatilia mahojiano haya kupitia mtandao wa Youtube wa PMTV