Mswati akanusha nchi yake kuwa na uhaba wa wanaume
Eric Buyanza
March 12, 2024
Share :
Serikali ya Mfalme Mswati imekanusha taarifa iliyokuwa ikisambaa kwa kasi kwamba ilikuwa ukitoa uraia kwa wanaume kutoka kusini mwa Afrika ili kuziba pengo la uhaba wa wanaume nchini humo.
Hiyo inafuatia barua inayodaiwa kuwa feki iliyoandikwa na Mfalme Mswati akielezea wasiwasi wake kuhusu 'uhaba wa wanaume' nchini mwake.
Barua hiyo ilidai mfalme angewezesha wanaume walio tayari kutoka kusini mwa Afrika kuoa wake na kupata nyumba za bure nchini humo.
"Umma unaarifiwa kuwa tangazo linalosambaa ni feki" serikali ya nchi hiyo ilisema katika taarifa fupi iliyotumwa kwenye mtandao wa X (zamani Twitter).
Haijabainika ni nani aliyesambaza taarifa hizi zilizowasisimua baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoka kusini mwa Afrika.