Mtangazaji atangaza kuumwa saratani akiwa mubashara
Sisti Herman
January 9, 2024
Share :
Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha nchini Marekani CNN aitwaye Sara Sidner wakati anamaliza kusoma taarifa ya habari sabuhi ameweka wazi kuwa anasumbuliwa na saratani ya matiti.
Sara amesema ameweka wazi kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa lengo la kuwataka wanawake wengine kufanya vipimo vya afya zao kila mwaka huku akieleza kuwa yupo katika matibabu mwezi wa pili sasa, na ugonjwa wake ukiwa hatua ya tatu.
Tukio hilo limetokea siku ya jana Jumatatu, wakati alipokuwa akiripoti moja kwa moja katika kipindi cha asubuhi cha CNN News Central.