Mtanzania kidedea mashindano ya kupiga makasia Hispania
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Mtanzania Emanuel Moses Onasaa ameibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Mchezo wa Kupiga Makasia Majini (PADDLE SURF) yaliyofanyika katika mkoa wa Aragon nchini Hispania Machi 16, 2024.
Mchezo huo wa kupiga makasia majini umejipatia umaarufu katika nchi mbalimbali za Ulaya, Marekani na Asia hatua iliyomfanya Bw. Emanuel Moses Onasaa kuwa Mwafrika pekee aliyefanikiwa kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya ngazi, kitaifa nchini Hispania mwaka 2023.