Mtanzania kucheza Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao.
Joyce Shedrack
July 17, 2024
Share :
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Aisha Masaka ametambulishwa rasmi na klabu ya Brighton Hove Albion inayoshiriki Ligi Kuu ya wanawake Nchini Uingereza akitokea Bk Hscken ya Nchini Sweden.
Huwenda Masaka akawa mchezaji pekee atakayecheza Ligi Kuu ya Wanawake Uingereza msimu ujao kutokana na kuwa Muafrika pekee aliyetangazwa kucheza katika ligi hiyo msimu ujao.
Masaka aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa ya wanawake barani Ulaya akiwa na Bk Hscken na kuishia hatua ya Robo Fainali.
Kama hakutakuwa na Klabu nyingine itakayomtambulisha mchezaji wa Afrika kwenye Ligi hiyo basi Masaka atakuwa mchezaji pekee wa Afrika anayekiwasha ligi kuu Nchini humo.