Mtoto aliyeuzwa na mama yake kwa laki 7, aokolewa
Eric Buyanza
July 10, 2024
Share :
Huko nchini Nigeria, mtoto wa kiume wa wa miaka 3 aliyetambulika kwa jina la Friday Okonkwo, ambaye aliuzwa kwa Naira 410,000 (sawa na shilingi laki 7 za kitanzania) ameokolewa na polisi.
Kwa mujibu wa polisi, mtoto huyo aliuzwa na mama yake mzazi aitwae Blessing Okonkwo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alitaka apewe kiasi hicho cha fedha zikamsaidie kuanzisha biasahara.