pmbet

Mtoto aokolewa baada ya kukaa chini ya vifusi kwa saa 14

Eric Buyanza

November 23, 2026
Share :

Mvulana mwenye umri wa miaka saba anayefahamika kwa jina la David ameokolewa akiwa hai baada ya kukaa kwa takriban saa 14 chini ya kifusi cha jengo la makazi lililoporomoka kufuatia shambulio la anga la Urusi katika mji wa Dymer, uliopo katika eneo la Kyiv nchini Ukraine.

 

Kwa mujibu wa taarifa za vikosi vya uokoaji na vyombo vya habari nchini humo, mtoto huyo alitolewa kwenye mabaki ya jengo hilo la ghorofa tano akiwa katika hali ya utulivu na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu. Licha ya kukaa kwenye kifusi kwa muda mrefu, waokoaji walishangazwa na ujasiri wake baada ya kusikika akiwaambia, "Msiharakishe, niko sawa!"

 

Shambulio hilo la usiku wa kuamkia Jumapili lililotekelezwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni) lilisababisha uharibifu mkubwa na kuua takriban watu 11, huku wengine sita wakijeruhiwa. Mbali na mvulana huyo, Mkuu wa Utawala wa eneo la Kyiv, Tymur Tkachenko, alithibitisha kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 79 naye aliokolewa akiwa hai kutoka kwenye kifusi hicho na kupelekwa hospitalini.

 

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa shughuli za uokoaji zilikuwa ngumu kutokana na ving'ora vya tahadhari ya mashambulizi mapya vilivyokuwa vikilia mara kwa mara.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet