Mtoto atolewa (screw) iliyokwama kwenye mapafu yake
Eric Buyanza
January 24, 2024
Share :
Mtoto ametolewa Skrubu (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera na kwenda kuinasa na kisha kuitoa ambayo alikua akiichezea kinywani mwake wakati akiwa shuleni na hatimaye kumpalia na kisha kukwama na kushindwa kutoka.
Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mwanaada Kilima anasema mtoto huyo alipaliwa na skurubu hiyo siku nne zilizopita ambayo iliyoingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa sana na kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida.
Bw. Msafiri Chatanda, mzazi wa mtoto huyo amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa waliyofanya tangu alipofikishwa hospitali hapo na kufanikisha kutoa skurubu hiyo.
Bw. Chatanda amewaasa wazazi kuwa watoto wamekuwa na desturi ya kuchezea vitu lakini hakuna mzazi anaangaika kumkumbusha mtoto madhara yake na kuona kuwa ni kitu cha kawaida.