Mtoto mwenye ualbino auawa na kunyofolewa viungo
Eric Buyanza
June 18, 2024
Share :
Zikiwa zimepita wiki takriban mbili na zaidi, baada ya mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novarti kuchukuliwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao katika Kijiji cha Mbale, Muleba mkoani Kagera, amekutwa ameuawa na mwili wake kufungwa kwenye kiroba na kutelekezwa kwenye karavati.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba, Benjamin Richard Mwikasyege amesema, baada ya kuripotiwa kuonekana kwa mfuko uliokuwa umefungwa mwili wa mtoto huyo, wamekuta baadhi ya viungo vya mwili wake havipo na kwasasa mwili huo umechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.