Mtoto wa Angelina Jolie apata ajali ya Pikipiki.
Joyce Shedrack
July 30, 2024
Share :
Mtoto wa mwigizaji Angelina Jolie, Pax Jolie-Pitt mwenye umri wa miaka 20 amepata ajali jioni jana Jumatatu wakati alipokuwa akiendesha pikipiki kwenye barabara ya Los Feliz Blvd Carlifonia Nchini Marekani.
Kijana huyo ambaye ni mtoto wa nne kwa mwigizaji huyo alipata ajali hiyo baada ya kugongwa na gari nyuma na kusababisha kupata majeraha kichwani yaliyomuweka chini ya uangalizi wa madaktari mpaka sasa.
Pax ambaye kwa wiki sasa ameonekana akiendesha pikipiki hiyo aina ya BMX amepata jeraha hilo la kichwa kutokana na kutovaa kofia maalum ya pikipiki yaani helment.