pmbet

Mtoto wa Binti mfalme ahukumiwa jela kwa ubakaji

Eric Buyanza

June 15, 2026
Share :

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Juni 15, 2026, na Mahakama ya Wilaya ya Oslo nchini Norway.
 

Høiby (29), ambaye ni mtoto wa kambo wa mkuu wa ufalme wa Norway (Crown Prince Haakon), alikuwa anakabiliwa na jumla ya mashtaka 40, yakiwemo makosa manne ya ubakaji.

 

Majaji watatu wa mahakama hiyo walimkuta na hatia ya makosa mawili ya ubakaji.

Moja ya matukio hayo lilifanyika mwaka 2018 ndani ya makazi rasmi ya familia ya kifalme (Skaugum).

 

Mahakama imemuondolea hatia katika mashtaka mengine mawili ya ubakaji kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha

Mbali na ubakaji, amepatikana na hatia ya unyanyasaji dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake (Nora Haukland), kutoa vitisho, na makosa ya dawa za kulevya
 

Upande wa mashtaka ulikuwa umeomba afungwe miaka saba na miezi saba, wakati mawakili wake walitaka asifungwe zaidi ya miezi 18. Hata hivyo, Høiby ambaye alikanusha mashtaka makubwa ya ubakaji wakati wa kesi hiyo, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hii.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet