pmbet

Mtoto wa Carlo Ancelotti ateuliwa kuwa kocha mkuu wa Lille.

Joyce Shedrack

June 1, 2026
Share :

Klabu ya Lille ya ligi kuu Nchini Ufaransa imemtangaza mtoto wa Carlo Ancelotti, Davide Ancelotti kuwa kocha wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili.

Davide Ancelotti è pronto per fare l'allenatore

Ancelotti mwenye umri wa miaka 36, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, atakuwa akichukua jukumu lake la pili la ukocha mkuu baada ya kuhudumu kwa miezi mitano kama kocha wa klabu ya ligi kuu ya Brazil, Botafogo, mwaka uliopita.

 

Davide alianza kazi yake ya ukocha mwaka 2016 na amefanya kazi bega kwa bega na baba yake Carlo katika vilabu vya Napoli, Bayern Munich, Everton, na Real Madrid akiwa kocha msaidizi.

 

Kwa sasa pia anahudumu kama kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Brazil, mabingwa wa dunia mara tano, baada ya kujiunga na benchi la ufundi la baba yake mwaka 2025.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet