Mtoto wa kwanza 2024 apewa jina la Mbappe
Sisti Herman
January 12, 2024
Share :
Mtoto wa kwanza kuzaliwa mwaka 2024 nchini Hispania amepewa jina la mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya Taifa ya Ufaransa, KylianMbappe.
Wazazi wa mtoto huyo wajulikanao kama Fran Barreiro na Jenny Gallego, wamempa jina la ‘Kylian’ mtoto wao kama heshima kwa mchezaji huyo kutokana na baba yake kuwa shabiki kindaki ndaki wa Mbappe.
Aidha mtoto huyo anatajwa kuwa wa kwanza kuzaliwa kwa mwaka 2024 nchini Hispania katika hospitali ya Alvaro Cunqueiro ambapo alizaliwa Januari 1 akiwa na uzito wa kilo 3.45.