pmbet

Mtoto wa Mbowe ashangazwa na tangazo nje ya nyumba yake

Eric Buyanza

February 29, 2024
Share :

Dudley Mbowe, ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe jana alipatwa na mshangao na kutoridhishwa na kitendo cha Dalali wa Mahakama, Jesca Massawe, kufika nyumbani kwake Mikocheni na kubandika tangazo la kupigwa mnada kwa nyumba hiyo kutokana na deni la Shilingi milioni 62.7.
 

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, ilitoa amri ya kupigwa mnada nyumba hiyo na kumteua Jesca Massawe, kutoka Kampuni ya Udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors, kutekeleza amri hiyo.
 

Tukio hilo limetokea jana ambapo Jessica aliripoti Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mikocheni A, ilipo nyumba hiyo na kisha kubainisha notisi aliyoibandika nyumbani kwa Dudley.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet