pmbet

Mtoto wa miaka 2 afariki kwa kujipiga risasi, wazazi wake wakiwa dukani

Eric Buyanza

July 10, 2024
Share :

Huko Douglas, Georgia nchini Marekani, mtoto wa miaka 2 aliyefahamika kwa jina la Nakyzi Odums, amefariki dunia baada ya kujipiga risasi kimakosa kwa kutumia bunduki ya wazazi wake iliyosahaulika kwenye gari wakati wazazi wake wakiwa dukani siku ya Julai 3.

Mashuhuda wamesema wazazi hao wakiwa dukani walisikia mlio wa risasi na kukimbilia kwenye gari ambapo walimkuta mtoto huyo akiwa na jeraha kubwa kifuani kwake.

Mtoto huyo alikimbizwa hospitali ya karibu kwa ajili ya kuokoa maisha yake lakini alifariki siku ya Jumamosi ya Julai 6.

Haijajulikana bado kama wazazi hao watakabiliwa na mashtaka yoyote kuhusiana na kifo cha mtoto huyo. 

Mkuu wa Polisi wa Douglas. Brannen Pruette aliliambia gazeti la The Independent: 

“Unaruhusiwa kuwa na bunduki ndani ya gari, lakini kunapokuwa na mtoto unapaswa kuhakikisha kuwa bunduki hiyo iko sehemu salama ili mtoto asiione.”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet