pmbet

Mtoto wa miaka 8 ajinyonga kisa ugomvi wa wazazi

Eric Buyanza

March 19, 2024
Share :

Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Maisaka mjini Babati, mwenye umri wa miaka nane, anadaiwa kujinyonga kutokana na kudaiwa kuchukizwa na ugomvi kati ya baba na mama yake.
 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mtaa wa Mruki, Abdilahi Rajabu, amesema tukio hilo limetokea Machi 16 mwaka huu majira ya saa saba mchana ikiwa ni siku ya nne tangu mama mzazi wa marehemu aondoke nyumbani kutokana na ugomvi wa kila mara kati ya wazazi hao.
 

Inasemekana kuwa Adam Abdala ambaye ni baba wa mtoto huyo amekuwa na ugomvi na mkewe mara kwa mara kutokana na wivu wa kutoaminiana na kwamba wamekuwa wakigombana mbele za watoto hata mara ya mwisho Adam alimnyang'anya mkewe ufunguo wa nyumba mbele za watoto.
 

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, baba wa mtoto huyo amekiri kuwepo ugomvi kati yake na mkewe na kwamba ni kweli watoto walikuwa wanafahamu tofauti kati yake na mkewe lakini hakutarajia kufikia hatua hiyo.
 

Hata hivyo mwili wa mtoto huyo umechukuliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati uchunguzi ukiendelea.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet