pmbet

Mtoto wa Mr Ibu akamatwa akidaiwa kuiba michango ya matibabu

Eric Buyanza

January 27, 2024
Share :

Polisi nchini Nigeria wanamshikilia mtoto wa kiume na binti wa kambo wa muigizaji maarufu wa vichekesho wa Nigeria John Okafor, maarufu Mr Ibu, kutokana na madai kuwa waliiba pesa zilizokusudiwa kwa matibabu ya muigizaji huyo.
 

Onyeabuchi Okafo na Jasmine Okekeagwu wanadaiwa kwa kutumia simu ya muigizaji huyo wakati anaumwa waliingilia miamala ya benki na kuiba Naira milioni 55.
 

Pesa hizo ni sehemu ya fedha ambazo zilikuwa zimechangwa na mashabiki na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya matibabu ya muigizaji huyo, baada ya kuugua kwa muda mrefu mwaka jana...ugonjwa ambao ulisababisha kukatwa kwa mguu wake mmoja.

Washukiwa hao wawili walikuwa wakipanga kutorokea Uingereza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet