Mtoto wa rapa AKA ashinda tuzo ya mtoto mwenye ushawishi Afrika.
Joyce Shedrack
July 19, 2024
Share :
Mtoto wa Marehemu rapa wa Afrika Kusini AKA Kairo Forbes ameshinda tuzo ya mtoto Mwenye ushawishi zaidi Afrika huku akiweka wazi ndoto yake ya kuwa mwanamitindo mkubwa duniani.
Kairo mwenye umri wa miaka 9 hii siyo mara yake ya kwanza kushinda tuzo kwani mwaka jana alishinda tuzo ya mtoto mwenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kutoka nchini Afrika Kusini.
Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Kairo alisema anamshukuru Mungu, familia yake na watu wote waliomuunga mkono na kama baba yake angekuwa hai angesema ni jinsi gani anajivunia yeye na kazi kubwa aliyoifanya.
Rapa AKA alifariki tarehe 11 february mwaka 2023 akiwa na umri wa miaka 35 kwa kupigwa risasi akiwa nje ya mgahawa wa Coastal City katika mji Durban nchini humo.