Mtoto wa Ronaldo ajifua kwenye Academy ya Madrid
Eric Buyanza
March 25, 2026
Share :
Imeripotiwa kwamba mtoto mkubwa wa Cristiano Ronaldo anafanya mazoezi na akademi ya vijana ya Real Madrid kwa nia ya kujiunga na kilabu katika siku za usoni.
Ronaldo Jr inasemekana amefanya mazoezi na kikosi cha Merengues chini ya umri wa miaka 16 kabla ya kuhamia La Fabrica siku za usoni.
Ronaldo Jr. ambaye anacheza kama mshambuliaji, kwa sasa ni sehemu ya akademi ya Al Nassr, akisaini huko baada ya baba yake kujiunga na wababe hao wa Saudi Arabia mnamo Desemba 2022. Kabla ya hapo, kijana huyo alicheza kwenye timu za vijana za Juventus na Manchester United, vilabu vingine viwili vya zamani vya Cristiano.






