pmbet

Mtoto wa Wayne Rooney alamba mkataba Man U.

Joyce Shedrack

February 6, 2026
Share :

Mtoto wa Wayne Rooney, Kai, amepewa mkataba mpya na Manchester United, ambapo anatumai kufuata nyayo za baba yake maarufu,hii ni kulingana na ripoti nchini Uingereza.
Manchester United sign Wayne Rooney's 11-year-old son Kai to academy | The  Independent

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 16, ambaye anamaliza shule wakati wa kiangazi, amekuwa katika akademi ya United kwa miaka kadhaa na klabu hiyo imevutiwa na maendeleo yake.
 

Kuna uwezekano mkubwa kwamba ufadhili wa masomo utatolewa kwa kijana huyo wakati wa kiangazi au usiku wa kuamkia msimu mpya, huku mkataba wa pauni 50,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Milioni 150 kwa mwaka ukitarajiwa, kulingana na gazeti la The Sun.

 

Kai anasemekana kuwa sehemu ya kundi 'lenye nguvu sana' la vijana 14 wanaopewa mikataba mipya na klabu hiyo.

Kundi hilo lenye vipaji pia linamjumuisha Jacey Carrick mwana wa Michael, ambaye ni meneja wa muda wa United.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet