pmbet

Mtu anaweza kuoa hata mara 50 - Yul Edochie

Eric Buyanza

June 10, 2024
Share :

Kutoka kiwanda cha filamu za Nigeria (Nollywood), muigizaji mtata Yul Edochie anasema hakuna ubaya kuachana na ndoa ambayo unaona haikupi furaha, na kusisitiza kuwa mwanaume unaweza kuoa hata mara 50 ilimradi tu ukae kwenye ndoa inayokupa furaha.

Edochie anaendelea kubainisha kuwa linapokuja suala la ndoa, ni kuhusu furaha ya mtu binafsi na si maoni ya umma.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi majuzi Edochie alisema ni sawa pia kukaa bila kuoa au kuolewa ikiwa inakufurahisha.

“Kwangu mimi, ndoa si kitu cha muhimu saanaaa. Ikiwa unaona ndoa haifanyi kazi, ondoka kwa heshima. Hakuna haja ya kuumizana. Na ukienda mbali ukakutana na mtu mwingine na ukaamua kuoa, endelea. Ukiona haifanyi kazi na yenyewe...funga ndoa nyingine. Unaweza kuoa hata mara 50 ili mradi inakupa furaha.

"Huwezi kudhibiti jinsi watu wanavyokuchukulia....na kinachonifurahisha ni tofauti na kile kinachokufurahisha wewe."

"Usiruhusu mtu yeyote akuambie kile kinachofaa kwako. Kijue kinachokufaa wewe mwenyewe"

"Na ikiwa utaamua katika maisha haya kwamba hutaoa hadi kufa, tafadhali fanya. Kuwa na furaha."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet