pmbet

Mtu kuwa mwembamba hakumaanishi ni mgonjwa - Janabi

Eric Buyanza

March 6, 2024
Share :

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema mtu kuwa mwembamba haina maana kwamba ni mgonjwa, akionya unyanyapaa dhidi ya kundi hilo ambalo yeye ni sehemu yake.
 

Prof. Mohamed Janabi, amesema unyanyapaa upo hata miongoni mwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU), akieleza alivyoshuhudia hali hiyo wakati anatoa matibabu kwa kundi hilo.
 

Amesema alipokuwa anatoa matibabu kwao, wengi wao walimwona anafaa kuwatibu, wakiwakataa madaktari wengi kutokana na yeye (Janabi) kuwa mwembamba.
 

“Kilichonisikitisha, kwanini wagonjwa wengi wanaletwa kwangu?......Nikavumilia ila siku nikamwuliza muuguzi mkuu ‘mbona wagonjwa wengi mnawapangia kwangu?’ Akasema wagonjwa wenyewe wanasema ‘wewe ni mwathirika mwenzao, wanakuwa na faraja zaidi ukiwatibu wewe’,” amesema Prof. Janabi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet