Mtu wa saba huenda akawa 'amepona' virusi vya Ukimwi kabisa
Eric Buyanza
July 19, 2024
Share :
Mwanaume mmoja wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 60, huenda akawa mtu wa saba kupona Virusi vya Ukimwi baada ya kupandikizwa Uloto.
Mjerumani huyo, ambaye ametaka kutotajwa majina, amepachikwa jina la "Mgonjwa anayefuata wa Berlin".
DW inaripoti kuwa Daktari mtafiti katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Charite cha Berlin Christian Gaebler, amesema timu yao hata hivyo haiwezi kuthibitisha kwa uhakika ikiwa virusi vya VVU vimetokomezwa kabisa kwa mgonjwa huyo.