pmbet

Mtukufu Aga Khan IV afariki dunia

Sisti Herman

February 5, 2025
Share :

Kiongozi Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Mtukufu Aga Khan anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, alifariki dunia jana Jumanne Februari 4, 2025, jijiji Lisbon, Ureno akiwa amezungukwa na familia yake.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa umma, baada ya kifo cha mfalme huyo, Imamu wa 50 wa madhehebu ya Shia Ismailia atatangazwa kurithi mikoba ya Aga Khan IV.

Enzi za uhai wake, Mtukufu Aga Khan alifahamika kutokana na mchango wake kwenye shughuli zinazochangia kuimarisha ustawi wa maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Mtukufu Aga Khan ameacha nembo isiyofutika maeneo mbalimbali duniani hususan nchini Kenya na Tanzania ambako alianzisha taasisi mbalimbali zilizoleta mchango mkubwa katika maisha ya raia wa nchi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet