Mtumbwi walipuka moto, wawili wahofiwa kupoteza maisha Ziwa Victoria
Eric Buyanza
April 1, 2024
Share :
Watu wawili wa familia moja, wakazi wa Majita, Wilaya ya Musoma Vijijini, mkoani Mara wanahofiwa kufariki dunia na wengine wawili kunusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wanatumia katika shughuli za uvuvi katika Kisiwa cha Gosba na Ukara ndani ya Ziwa Victoria kulipuka moto.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mtumbwi waliokuwa wanatumia ulilipuka na kuwaka moto baada ya mpira wa tanki la mafuta ya petroli kuchomoka na kusababisha mafuta kusambaa ndani ya mtumbwi huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kinyang’wena, Seleman Makanje amethibitisha kutokea tukio na kusema kuwa baada ya mafuta hayo kusambaa yalikutana na jiko la moto walilokuwa wakilitumia kupika ndani ya mtumbwi huo na kusababisha mlipuko huo.