pmbet

Mtwara kumekucha, Bandari sasa kushusha makontena 25 kwa saa!

Eric Buyanza

February 12, 2024
Share :

Bandari ya Mtwara ambayo ina uwezo wa kuhudumia tani milioni moja za shehena kwa mwaka, imepata mtambo wa kisasa uitwao 'Ship to Shore Gantry Crane (SSG)', wenye uwezo wa kuhudumia makontena 25 kwa saa.
 

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Bandari hiyo, Ferdinand Nyathi, wakati akiwaeleza wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu maboresho yanayofanyika kwenye bandari hiyo.
 

Alisema mtambo huo wa SSG tayari umeshasimikwa na kuongeza kuwa mbali na hiyo pia wamepata scanner moja yenye uwezo wa kuhudumia makontena 30 kwa saa.
 

Alisema hayo yametokana na maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye bandari hiyo yakihusisha pia ujenzi wa gati moja la nyongeza lenye kina cha mita 13 na urefu wa mita 300.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet