pmbet

Muadhin wa Makkah afariki dunia muda mfupi baada ya Adhana ya mwisho

Sisti Herman

September 22, 2026
Share :

 

Muadhini wa Msikiti mkuu wa Makkah, Masjid Al-Haram, Sheikh Ibrahim Al-Madani jana alifariki dunia saa chache tu baada ya kutangaza adhana yake ya mwisho mjini Makkah.

Sheikh Ibrahim Al-Madani, mmoja wa waadhini wa msikiti mtakatifu zaidi katika Uislamu, alifariki dunia alfajiri ya Jumatatu, tarehe 21 Septemba.

Saa chache kabla ya hapo, Sheikh Ibrahim alikuwa ametangaza adhana ya kwanza ya Alfajiri (Fajr) katika Masjid Al-Haram, ambayo ikawa mwito wake wa mwisho wa kusali.

Picha za video zilizosambazwa baada ya kifo chake zilionyesha sauti yake ikisikika kwa mwangwi ndani ya Msikiti Mkuu na kuzunguka Kaaba.

Sheikh Ibrahim alihudumu kama muadhini rasmi wa Masjid Al-Haram tangu mwaka 1439 Hijria (takriban 2017–2018), na alijulikana sana kwa adhana yake ya Alfajiri, takbira za Eid, na sauti yake ya kipekee. 

Safari yake kama muadhini ilianza akiwa na umri wa miaka 15 tu mjini Madinah.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet