Muda wa Tanzania kuishangaza Dunia.
Joyce Shedrack
May 16, 2026
Share :
Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 Tanzanite Queens imepangwa kundi B kwenye michuano ya Kombe la Wanawake ikiwa pamoja na Brazil,Canada pamoja na Uingereza.

Tanzanite Queens ambayo ilifuzu michuano hiyo baada ya kuiondosha Cameroon kwa faida ya goli la ugenini kufuatia sare ya mabao 3-3 itashiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo itakayofanyika Nchini Poland.
Licha ya ugumu wa kundi ambalo Tanzanite Queens lakini bado wananafasi ya kwenda kufanya vizuri kwenye michuano hiyo na kuishaza Dunia kama ilivyowahi kufanya hivyo Nigeria 2010 na 2014 na kufanikiwa kufika Fainali ya Michuano hiyo.
Unadhani Tanzania itafanikiwa kufika hatua gani kwenye michuano hiyo?





