Mudathir Yahya kuikosa Kariakoo derby Mei 03.
Joyce Shedrack
April 20, 2026
Share :
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemfungia michezo mitatu kiungo wa Yanga SC, Mudathir Yahya kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji, Ibrahim Abraham wakati mchezo unaendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, mwanzoni mwa mwezi huu.

Kufungiwa huko kwa Mudathir kunamfanya alikose pambano la watani ambalo limepangwa kuchezwa Mei 03 katika Uwanja wa Benjanin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Licha ya Mudathir kuikosa michezo hiyo mitatu kwa kosa hilo, lakini pia atatakiwa kulipa faini ya kiasi cha Sh. Mil 1,000,000 (Milioni moja).





