Mudryk kurejea uwanjani baada ya miezi 20.
Joyce Shedrack
August 4, 2026
Share :
Mykhailo Mudryk anatarajiwa kurejea uwanjani Jumatano baada ya kukaa nje ya mchezo kwa takribani miezi 20, kufuatia kujumuishwa kwenye kikosi cha Chelsea kitakachocheza dhidi ya Juventus katika mechi ya kirafiki mjini Hong Kong.

Nyota huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 25 hajacheza mechi ya ushindani tangu Novemba 2024, baada ya kusimamishwa kwa muda kufuatia kukutwa na dawa iliyopigwa marufuku aina ya meldonium kwenye vipimo vyake.
Hata hivyo, wiki iliyopita aliruhusiwa kurejea uwanjani baada ya kumaliza mchakato wa kesi yake na Chama cha Soka cha England (FA).
Kocha mpya wa Chelsea, Xabi Alonso, amesema:
"Ndiyo, anaweza kucheza. Dakika 90 zinaweza kuwa mapema kwake, lakini yupo kwenye kikosi na anaweza kutumika."





