Muhimbili yaingia 3 bora vyuo vikuu bora Afrika
Sisti Herman
May 31, 2024
Share :
Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili cha Tanzania kimetajwa kushika nafasi ya tatu kwa ubora kusini mwa jangwa la Sahara kwenye ripoti iliyotolewa na Times Higher Education imeorodhesha vyuo vikuu bora katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kwenye Orodha hiyo pia mbali na Muhimbili pia chuo kikuu cha Ardhi kimetajwa kwenye nafasi ya 10.
Hivi ni vyuo vikuu bora katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mujibu wa Times Higher Education;
1.Chuo Kikuu cha Witwatersrand – Afrika Kusini
2.Chuo Kikuu cha Johannesburg – Afrika Kusini
3.Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – Tanzania
4.Chuo Kikuu cha Pretoria – Afrika Kusini
5.Chuo Kikuu cha Makerere – Uganda
6.Chuo Kikuu cha Western Cape – Afrika Kusini
7.Covenant University – Nigeria
8.UGHE – Chuo Kikuu cha Usawa wa Afya Ulimwenguni – Rwanda
9.Chuo Kikuu cha Ashesi – Ghana
10.Chuo Kikuu Ardhi – Tanzania
Orodha hiyo inalenga kuangazia taasisi za elimu ya juu barani Afrika pamoja na kushughulikia changamoto za elimu ya juu katika eneo hilo.