pmbet

Muhimbili yapokea msaada wa vifaa kutoka Qatar

Sisti Herman

April 20, 2025
Share :

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa viti mwendo 110, viti 30, meza 30, mashine za kupimia shinikizo la damu 30 na vifaa vingine vyenye thamani ya TZS. 52 Mil. kutoka shirika la Qatar Charity (QC) ili kusaidia utoaji huduma bora kwa wananchi.

Mkurugenzi Mkazi wa QC nchini Bw. Amjad Al Tahhan, amesema kuwa ni dhamira ya muda mrefu ya shirika hilo kutoa mchango wake ili kuinua jamii kwa kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji safi na fursa za kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilala na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu ambaye alikua mgeni rasmi katika kukabidhi msaada huo amesifu mchango wa QC katika shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii na kuongeza kuwa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za afya, elimu, na ustawi wa jamii.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi ameishukuru QC kwa mchango huo ambao utasaidia wananchi wengi wanaokuja kupata huduma hospitalini hapo ikiwemo watoto wa saratani ambao hukaa muda mrefu ambao watatumia viti na meza kwenye madarasa yao huku wakiwa wanatibiwa na kuendelea na masomo.

“Viti mwendo, vitasaidia jitihada za kuhudumia wananchi hasa wale ambao hawawezi kutembea kwani tunayo huduma ya kusaidia wananchi wanaoshuka kituo cha daladala ambao hawawezi kutembea na tuliajiri vijana kuhudumia wagonjwa hao ambao mara tu wanaposhuka kituo cha mabasi, hupata huduma hiyo kwa kupelekwa kituo husika cha kupata huduma ikiwemo kwenye vipimo vya maabara, radiolojia, kliniki ya wagonjwa wa nje, tiba kwa njia ya mazoezi n.k”, amesisitiza Prof. Janabi

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet