Muigizaji mkongwe wa nigeria, Amaechi Muonagor afariki dunia
Eric Buyanza
March 25, 2024
Share :
Msanii nguli wa filamu na sanaa za vichekesho kutoka Nigeria, Amaechi Muonagor amefariki dunia jana Jumapili akiwa na umri wa miaka 62.
Kifo cha msanii huyo kinaelezwa kuwa kimetokana na kushindwa kwa figo zake kufanya kazi na alikuwa kwenye matibabu ya dialysis (kusafishwa damu).
Siku chache zilizopita msanii huyo aliomba msaada wa fedha kwa ajili ya kwenda kupandikzwa figo nchini India.
Kifo chake kinakuja wiki chache tu baada ya Nigeria kumpoteza nyota mwingine wa Nollywood John Okafor (Mr. Ibu).