Muigizaji wa Batman afariki akiwa na umri wa miaka 65
Eric Buyanza
April 2, 2025
Share :
Muigizaji Val Kilmer, ambaye aliigiza katika baadhi ya filamu kubwa zaidi za miaka ya 1980 na 90, zikiwemo Top Gun na Batman Forever, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65.
Alionekana pia katika The Doors ya 1991, akicheza kama kiongozi wa bendi maarufu Jim Morrison, pamoja na Western Tombstone na tamthilia ya uhalifu Heat.
Kilmer alifariki kwa ugonjwa wa homa ya mapafu siku ya Jumanne huko Los Angeles, binti yake Mercedes aliviambia vyombo vya habari vya Marekani.
Alisema baba yake aligundulika kuwa na saratani ya koo mwaka 2014 lakini alipata nafuu baadae.
Upasuaji kwenye koo uliathiri sauti yake na kupunguza kasi yake kwenye uigizaji, lakini alirudi tena kwenye kazi hiyo kama rubani wa kivita kwenye movie ya Iceman pamoja na Movie ya Top Gun: Maverick ya mwaka 2022.