Muigizaji Zack Orji afanyiwa upasuaji wa kichwa
Eric Buyanza
January 4, 2024
Share :
Siku chache baada ya muigizaji maarufu wa nchini Nigeria Zack Orji kukimbizwa hospitali baada kuanguka chooni akiwa nyumbani kwake, taarifa zikufikie kuwa staa huyo amefanyiwa upasuaji wa kichwa.
Akiongelea kuhusu maendeleo ya afya ya Zack baada ya kumtembelea hospitali, Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Nigeria, Hannatu Musawa amewaomba wanigeria kuendelea kumuombea muigizaji huyo ili apate uponyaji kwa haraka.
“Tumemtazama akituburudisha, na tunamchukulia kama hazina ya taifa. Kwa hiyo, jambo bora tunaloweza kufanya ni kuhakikisha ya kwamba tunamuunga mkono katika kupata matibabu bora zaidi."
"Pia tunawaomba wanigeria waendelee kumuombea ili kuhakikisha kuwa anapona ugonjwa huu"
“Mungu atamponya. Tutafanya yote tuwezayo ili kumuunga mkono. Tunaomba maombi ya pamoja ya Wanaijeria.” alimalizia.