pmbet

Mume mahakamani kwa kutumia pilipili wakati wa faragha

Eric Buyanza

February 11, 2025
Share :

Huko jijini Harare nchini Zimbabwe kumetokea kisa cha ajabu baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Joyce Garikayi kumburuza mahakamani mumewe aliyefahamika kwa jina la Jack Mukandwe, akimtuhumu kwa unyanyasaji wa kutisha wa kutumia pilipili wakati wa tendo la ndoa na kumsababishia mwanamke huyo matatizo makubwa ya kiafya.

Joyce alidai kuwa mazoea ya Jack (mumewe) ya kutumia pilipili wakati wakiwa faragha yanamfanya apate shida sana. 

"Sehemu zangu za faragha kwasasa zimekuwa zikiniuma na kuniwasha sana kutokana na pilipili anayotumia mume wangu kwa kisingizio kuwa ni njia ya kunogesha mahaba wakati faragha. Kila nikikataa anakasirika na kunitukana sana,” Joyce aliiambia mahakama.

Cha kushangaza, Jack hakukataa tuhuma hizo badala yake alikubali na kusema alikuwa akifanya hivyo baada ya kujifunza kutoka kwa marafiki zake waliomwambia na wao wanatumia njia hiyo kunogesha mahusiano yao.

Jack aliomba radhi mahakamani hapo kwa vitendo vyake, huku uamuzi wa mahakama ukisisitiza kuna haja ya kumlinda Joyce dhidi ya madhara zaidi yanayoweza kutokea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet