pmbet

"Mume wangu kaniuliza, ningeolewa nae kama angekuwa fundi" - Regina Daniels

Eric Buyanza

January 8, 2024
Share :

Mwigizaji wa Nollywood Regina Daniels ameweka hadharani mazungumzo ya kufurahisha kati yake na mumewe, Seneta maarufu kwa jina la Ned Nwoko.
 

Regina anasema katika hali ya kushangaza siku moja akiwa kwenye mazungumzo na mumewe, alimuuliza swali lililomstaajabisha.

Swali alililoulizwa Regina na mumewe....."Je ungekubali kuolewa na mimi kama ningekuwa fundi magari?"
 

Regina anasema...."Nilicheka kwa kweli sikujua jibu nililopaswa kutoa, lakini nilimuuliza na mimi ‘Ungenionea wapi? Ninapokuja kutengeneza gari au?"
 

Regina wakati anaolewa mwaka 2019 alikuwa na umri wa miaka 22 na mumewe akiwa na miaka 61.

Wanandoa hao wamezaa watoto wawili pamoja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet