pmbet

Muna Love ajifungua mtoto mwingine wa kiume.

Joyce Shedrack

July 24, 2024
Share :

Msanii wa filamu za Bongo Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amejifungua mtoto  wa kiume baada ya kupitia maumivu  ya muda mrefu kufuatia kumpoteza mtoto wake wa kwanza wa kiume Patrick aliyefariki  Julai 3 mwaka 2018.

Muna Love amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na mtoto wake mchanga kwenye moja ya Hospitali nchini Canada na kuambatanisha na andiko lililowagusa wengi huku akimshukuru Mungu kwa kumpatia mtoto mwingine na kumkabidhi mikononi mwa Yesu akiahidi kuwa mtoto huyo atatumika kulitangaza jina la Yesu pamoja na mama yake.
 

Msanii huyo kupitia waraka huo amemshukuru marehemu mwanae Patrick kwa kumsaidia kumjua Yesu na  kumuomba radhi kwa kumlaumu kumuacha mapema huku akitangaza kumpata mtoto wa kiume aliyempa jina la "Testimony" akisema atampatia pia  jina lingine la Kiislamu ambalo atalitaja baadae ili mtoto huyo atumike kumtangaza Mungu katika dini zote.

“PATRICK naimani umefurahi nisamehe kwakukulaumu ni Uchungu na maumivu makali. YESU ASANTE KWA KUNIPA BABY BOY TENA,Kwakua Maisha yangu na hii Baraka imekuja kama majibu ya maombi yangu basi ataitwa (TESTMONY ) na JINA LINGINE LA MUSLIM NASUBIR NTASEMA" Baadhi ya maneno aliyoandika Munalove.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet