"Mungu nipe umaarufu ili wanaume wa kizungu wanipe pesa nyingi" - Moesha
Eric Buyanza
December 30, 2023
Share :
Muigizaji mtata kwelikweli kutoka nchini Ghana, mwenye figa inayowatoa udenda wanaume wengi wa kiafrika ameweka wazi kile anachotaka mungu amfanyie mwaka 2024.
Mwigizaji huyo aitwae Moesha Buduong, ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kujitapa kuwa maisha yake yanafadhiliwa na wanaume za watu (waliooa), safari hii ameibukia Instagram, akiomba kwa Mungu kuhusu mahitaji yake.
Kupitia Instagram ameandika.....“Mungu na anifanye kuwa mtu maarufu kwenye jamii, anayetafutwa zaidi ulimwenguni ili wanaume wa kizungu wanipe pesa nyingi ili nilale nao bila ngono....Ili kusudi niweze kuwa Malkia Elizabeth wa kivyanguvyangu.”