pmbet

Museveni amteua mtoto wake kuwa mkuu wa majeshi

Eric Buyanza

March 22, 2024
Share :

Rais Yoweri Museveni wa Uganda, amemteua mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa majeshi. 

Uteuzi huo hata hivyo umezua minong'ono huku wengi wakiamini kuwa Museveni anamsafishia njia mtoto wake ili aje kuwa Rais wa nchi hiyo. 

Muhoozi Kainerugaba anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jana jioni. 

Mtoto huyo wa kwanza wa rais amekuwa akifanya mikutano ya hadhara kote nchini, hatua ambayo inakwenda kinyume na sheria inayowazuia maafisa wa jeshi kujihusisha na siasa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet