pmbet

Museveni atoboa siri ya kutozuia mchele wa Tanzania

Eric Buyanza

January 13, 2024
Share :

Akiongea jana Januari 12, 2024 kwenye sherehe za kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesimulia jinsi alivyoukwepa mtego wa nchi yake kupiga marufuku mchele za Tanzania kuingia Uganda.
 

Hatua ya Museveni kutakiwa kupiga marufuku mchele ilikuja baada ya yeye kuambiwa na watu wake kuwa mchele huo umeua watu kadhaa wa Uganda.....lakini aligoma kuchukua hatua hiyo kwa kuwa yeye si kipofu.
 

“Nyuma kule Uganda waliniambia kwamba mpunga wa Tanzania umetuua huku Uganda, walikuwa wanataka nipige marufuku mchele wa Tanzania, nikasema siwezi kufanya hivyo, mimi si kipofu,” amesema.
 

“Nikifanya hivyo Serikali ya Tanzania nayo italipiza kisasi wanapiga marufuku hiki, mimi napiga marufuku kile, mchezo wa watoto siwezi kufanya namna hiyo,” amesema.
 

Kingine anasema kilichomfanya asichukue hatua hiyo, ni kulazimisha Waganda wanunue mchele wa bei ya juu ili kuwatetea wavivu wasiopenda kulima na kuleta ushindani wa uzalishaji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet