Museveni awaonya Gen Z wa Uganda "Wanacheza na moto".
Joyce Shedrack
July 21, 2024
Share :
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaonya Wananchi wanaopanga kufanya maandamano Julai 23, 2024 yanayolenga kupinga Vitendo vya Rushwa Nchini humo, wengi wakiwa ni Vijana wenye umri mdogo maarufu kama ‘Gen Z’.
Rais wa Nchi hiyo Yoweri Museveni wakati akihutubia Taifa hilo amewaambia vijana hao wanacheza na moto.
Museven amesema “Una haki gani unayotafuta kwa kuleta machafuko? Tuna shughuli nyingi za kuzalisha mali, unapata Chakula cha bei nafuu, sehemu nyingine za dunia wanakufa njaa wewe hapa unataka kutuvuruga? Unacheza na moto. Hatuwezi kukuruhusu utusumbue.”
Vijana wa Uganda ‘Gen Z’ wameonekana kuhamasika kutokana na kile kilichotokea Nchini Kenya kwa wiki kadhaa kundi la Gen Z kujitokeza kwenye maandamano yaliyochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko kwenye Uongozi wa Serikali ya Kenya kwa sasa.