Musiala afunguka baada ya kuzimia kwenye mechi 2 mfululizo
Sisti Herman
August 18, 2026
Share :
Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Jamal Musiala ametoa taarifa baada ya kuanguka tena uwanjani leo akiichezea Bayern Munich, akisema kuwa anaendelea vizuri.
Musiala anasema amegunduliwa kuwa na tatizo la kifafa cha aina ya 'transient absence seizures' na atatafuta ushauri pamoja na matibabu kutoka kwa wataalamu wa mfumo wa neva.
Musiala anasema kuwa hali yake inaweza kutibika kwa urahisi ana anatumai sana atapata nafuu haraka na kwamba watu watamheshimu katika kipindi hiki.
Picha kushoto ni waraka kwa mashabiki wake.





